Front page

MATANGAZO

KARIBU

Tuesday, January 21, 2014

FIFA yatoa onyo kwa wanaopanga matokeo

Shirikisho la Soka ulimwenguni FIFA limezitaka serikali za mataifa wanachama kusaidia kukomesha uhalifu wa kupanga matokeo ya mechi. Mkuu wa usalama katika shirikisho hilo Ralf Mutschke ameonya kuwa wachezaji watakaobainika kuhusika katika uhalifu huo watakabiliwa na adhabu ya kupigwa marufuku.
Kwa muda wa miaka kadhaa, wachezaji wengi wamesimamishwa kabisa kucheza soka baada ya kupatikana na hatia kama hiyo. Bwana Mutschke amesema wengi wa wachezaji hao ni wale wanaochezea vilabu vyenye matatizo ya fedha, na hufanya hivyo kutokana na dhiki baada ya miezi kadhaa bila malipo.Amesema Italia imepiga hatua kubwa katika kupambana na uhalifu kama huo, na kuongeza kuwa nchi nyingine za Ulaya hazina sheria mahsusi za kupambana na uhalifu wa kupanga matokeo ya mchezo.

No comments:

Post a Comment