Front page

MATANGAZO

KARIBU

Tuesday, January 7, 2014

Askofu Mkuu wa Sudan Kusini ataka amani

Kiongozi wa dini anayeheshimika sana nchini Sudan Kusini amesema kuwa hatma ya taifa hilo changa, iko mikononi mwa mahasimu wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya kumaliza mapigano nchini humo. Mkuu wa Baraza la Maaskofu, Askofu Mkuu, Daniel Deng Bul, amesema wananchi wa Sudan Kusini wanakufa kila siku bila sababu yoyote ile.


Amesema wanahitaji amani nchini humo na kwamba viongozi wanaoshiriki mazungumzo ya amani mjini Addis Ababa, Ethiopia, wanapaswa kusitisha mapigano. Ameuita mzozo unaoendelea kuwa usio wa maana na kutoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja, kwani wasipokubaliana sasa, hali inaweza ikawa mbaya zaidi. 

Mazungumzo ya ana kwa ana ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi yameanza mjini Addis Ababa jana Jumatatu, baada ya siku kadhaa za majadiliano ambako mahasimu hao walikutana kwa nyakati tofauti na wapatanishi kukubaliana kuhusu ajenda za mazungumzo.

No comments:

Post a Comment