BAADHI ya wakazi wa Dar es Salaam wanatumia vituo vya mabasi yaendayo kasi (DART) kama madanguro ya kufanyia ngono na sehemu za uporaji kwa vijana wa kihuni.
Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini vitendo vya ngono zembe vinafanywa na wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao kwenye vituo hivyo hasa sehemu za Magomeni, Manzese na Ubungo.
Eneo la Magomeni Mapipa ndilo lililoshamiri kwa vitendo vya ngono kuanzia majira ya usiku hadi alfajiri.Mbali na vitendo vya ngono, pia kumekuwa na matukio ya uporaji na ukabaji hasa kwa wakazi wanaopita maeneo hayo......HII HAIPENDEZI WATANZANIA KWANI NI KURUDISHA MAENDELEO NYUMA .ANZENI KUHESHIMU BAADHI YA MAENEO KWANI NI MALI YA TAIFA AMBALO WEWE MWENYEWE NDIYE MMILIKI HALALI KWA KODI ZAKO SI KUFANYA UCHAFU HUU....GOOD DAY
No comments:
Post a Comment