Maelfu ya polisi wa Afrika kusini watawekwa katika
eneo la tukio la kumbukumbu ya Nelson Mandela
katika uwanja wa kandanda wa mjini Soweto, na
maafisa watazuwia watu kuingia katika eneo hilo iwapo
watu watakuwa wengi kupita kiasi.
Waombolezaji ikiwa
ni pamoja na viongozi zaidi ya 70 kutoka kote duniani
wanatarajiwa kumiminika katika uwanja wa Soccer City
wenye uwezo wa kuingia watu 95,000. Mandela
alijitokeza mara ya mwisho katika uwanja huo siku ya
mwisho ya fainali za kombe la dunia mwaka 2010.
Luteni kanali Solomon Makgale, msemaji wa jeshi la
polisi nchini Afrika kusini , amesema kuwa polisi 1,000
wataelekeza magari, watawalinda waombolezaji na
watasaidia walinzi wa viongozi ambao watawasili nchini
humo kwa ajili ya tukio hilo.
Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuwasili nchini
Afrika kusini leo na kesho ni pamoja na rais Barack
Obama pamoja na mkewe Michelle Obama.
No comments:
Post a Comment