Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, December 26, 2013

Ujumbe wa Iran kwa Papa Francis I

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis I na Wakristo wote
kuadhimisha kwa kuzliawa kwa Yes Kristo. Miladia. Katika ujumbe wake wa pongezi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea matumaini yake kuwa, Papa Francis wa Kwanza atatumia cheo chake kusaidia kueneza amani, kupunguza umasikini na kujenga dunia isiyo na machafuko wala ubaguzi na wala misimamo mikali na kuelekea katika utulivu, uadilifu na msimamo wa wastani.Rais Rouhani ameashiria msimamo wa Papa Francis kuhusu udharura wa kuwepo mazungumzo baina ya dini mbali mbali na kuongeza kuwa, Papa Francis ana historia ya kufanya juhudi za mazungumzo baina ya madhehebu ya Kikristo na vile vile ushirikiano na mazungumzo na viongozi wa Kiislamu na Kiyahudi. Rais Rouhani amesema, juhudi za Papa Francis katika kupunguza umasikini na kuzuia kuenea masuala ya kimaada na utumizi mwingi wa bidhaa ni jambo linalotoa bishara ya kuweko muelekeo mpya kwa mtazamo wa kidini katika utatuzi wa masuala magumu duniani. Rais wa Iran ameongeza kuwa, kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu na Mitume wote wakubwa wa Mwenyezi Mungu ni fursa ya kuandaa mazingira ya kuwepo msingi wa kuheshimiana na mazungumzo baina ya dini ili kwa njia hiyo ya maelewano kupatikane moyo wa amani na kibinaadamu na hatimaye dini za Mwenyezi Mungu ziweze kukurubiana...IDHAA YA TEHRAN

No comments:

Post a Comment