Wanamuziki wawili waliokuwa gerezani wa bendi ya muziki nchini Urusi,ya Pussy Riot, wamesema bado wanataka kuona mwisho wa utawala wa rais Vladimir Putin.Nadezhda Tolok-onni-kova, na Maria Alyokhina, jana walifanya mkutano wao wa kwanza na waandishi habari tangu kuachiwa kwao huru kutoka kifungoni. Walifungwa kutokana na kuimba wimbo uliokuwa ukiikosoa serikali ya Urusi katika moja ya kanisa kuu la Yesu Mwokozi mjini Moscow. Wanamuzi hao waliachiwa huru Jumatatu iliyopita baada ya kutumikia kifungo cha miezi 21, katika hukumu yao ya miaka miwili gerezani. Nadezhda Tolok-onni-kova amesema kuachiwa kwao huru ni jitihada za Putin kuboresha taswira ya Urusi kabla ya michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi mjini SOCHI inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani nchini humo.
Moja ya maandamano kulaani kufungwa kwa kina dada hao yakiwa ya nusu utupu
No comments:
Post a Comment