Leo ni sikukuu ya Krismasi ambapo Wakristo wanaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo miaka 2,013 iliyopita. Kwenye makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican, Mkuu wa Kanisa hilo duniani, Baba Mtakatifu Francis, aliongoza ibada ya kwanza ya mkesha wa Krismasi hapo jana kwa kuwatolea wito Wakristo kufungua nyoyo zao na kupambana na nguvu za giza, alizozitaja kuwa ni ufahari, udanganyifu na ubinafsi. Nako mjini Bethlehem, Palestina, ambako inaaminika ndiko Yesu alikozaliwa, Askofu Mkuu Jerusalem, Fouad Twal, ametumia misa hiyo ya mkesha wa Krismasi kuelezea hofu yake ya kutokupatikana kwa suluhisho la mgogoro wa Israel na Palestina, licha ya kwamba eneo hilo linatambuliwa kuwa Ardhi Tukufu. Maelfu ya mahujaji kutoka duniani kote wamefurika kwenye eneo hilo la kusini mwa Ukingo wa Magharibi, kuadhimisha siku hii ya Krismasi.
No comments:
Post a Comment