Front page

MATANGAZO

KARIBU

Tuesday, December 10, 2013

ilipatwa kusemwa na itabaki kuwa kweli!!!!!....Utaliii chanzo muhimu cha ajira

MKURUGENZI WA JAMBO FESTIVAL AUGUSTINE MICHAEL
Serikali imeaswa kuwekeza katika utalii utokanao na vivutio vya Kijamii hasa maisha ya watu na vinavyowazunguka badala ya kuangalia kwa nguvu kubwa upande mmoja tu wa mbuga na mali asili.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi inayosimamia na kuhamasisha uhifadhi wa maisha ya kitamaduni pamoja na sanaa kwa ujumla wake yaani Jambo Festival Bwana Augustine Michael Namfua wakati akitoa tuzo maalum za kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja au nyingine walifanikisha tamasha la JAMBO FESTIVAL mwaka 2012. 


Amesema kuwa Watanzania wana kila sababu ya kunufaika na maisha yao ya asili kwa vile ndani yake kumekuwa na maadili, miiko , kuheshimiana, kushirikiana sambamba na kuonyesha vipaji kwa kutengeneza kazi za sanaa kama uhunzi, uchongaji wa vinyago, ususi, uchoraji, uimbaji, uchezaji ngoma, ufinyanzi, utungaji, ufumaji, tiba za asili, uandaaji wa vyakula vya asili n.k.


Bwana Augustine ameongeza kuwa kwa sasa taifa linapoteza pato kubwa kwa vile sanaa imekuwa kama vile jambo la ziada lisilo na maana wakati jamii kubwa hasa vijana wakibaki mitaani wakiwa wamebeba lawama kwa serikali.Katika utoaji wa tuzo hizo ambao umefanyika katika hotel yenye historia na heshima kubwa jijini Arusha yaani Arusha hotel ambayo ilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na wakoloni katika eneo ambalo ni katikati ya Afrika , ilitoa nafasi kwa wadau kadhaa ikiwemo kampuni ya Mega Trade Investment chini ya kinywaji chao cha K-Vant Gin kuchukua tuzo ya juu ya wadau waliojotoa kwa karibu zaidi.
Hata hivyo kwa upande wa Wasanii walikuwa wameshiriki katika tamasha hilo kwa Mwaka jana Worrios From The East pamoja na S.U.A nao pia walipata tuzo Maalum kwa ushiriki wao.

No comments:

Post a Comment