Saturday, December 28, 2013
Igad haitokubali kupinduliwa serikali ya Sudan Kusini
Nchi zilizo jirani na Sudan Kusini zimesema haziwezi kuruhusu vita vya kutaka
kuiondowa kwa nguvu madarakani serikali ya rais Salva Kiir iliyochaguliwa
kwa njia za kidemokrasia.Hatuwa hiyo imekuja baada ya takriban wiki mbili za
mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wale wanaomuunga mkono
makamu wake wa zamani.Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akizungumza katika
mkutano maalum wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya kiserikali ya ushirikiano
wa Maendeleo mashariki mwa Afrika -IGAD ametowa mwito kwa rais Kiir na
makamo wake wa zamani Riek Machar kutumia nafasi iliyopo na kuanzisha
mazungumzo ya amani.Rais Kenyatta amesisitiza kwamba vita sio suluhisho
la mgogoro katika taifa hilo changa.Mkutano huo wa IGAD unatarajiwa
kuanzisha mpango wa kusaka maridhiano kati ya rais Kiir na mpinzani wake
Riek Machar anayetuhumiwa kuanzisha jaribio la mapinduzi lililoshindwa na
ambalo serikali imesema ndiyo chanzo cha mapigano yanayoshuhudiwa
sasa Sudan Kusini...DW SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment