Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, November 29, 2013

Waandamanaji wavamia jeshi ......Mamia ya waandamanaji nchini Thailand waliingia kwa nguvu katika makao makuu ya jeshi mjini Bangkok, ikiwa ni siku ya sita tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya serikali.Msemaji wa jeshi amesema waandamanaji walivunja kufuli la mlango mkuu na kuingia katika eneo la makao makuu hayo ya jeshi. Baadaye waliondoka. Alhamisi, Waziri Mkuu Yingluck Shinawatra aliwataka waandamanaji kuacha maandamano mitaani, ikiwa ni baada ya waziri mkuu huyo kushinda kura ya kutokuwa na imani naye iliyopigwa bungeni.Lakini kiongozi wa waandamanaji Suthep Thaugsuban amekataa ombi hilo.

No comments:

Post a Comment