Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, November 15, 2013

ungana na Fred Mosha ufahamu kuhusu SALUM ABDALLAH

Novemba 19 itakuwa miaka 48 kamili bila Salum Abdallh. Huyu ni mwanamuziki ambaye kwa hakika dunia ya muziki wa Tanzania haitamsahau. Huyu Bwana jina lake kamili ni Salum Abdallah Yazid aliyezaliwa Mkoani Morogoro mwaka 1928. Mapenzi yake kwa muziki hasa wa latino yalikuwa makubwa kiasi cha kuwahi kufanya jaribio la kutoroka nchini kwenda kujifunza muziki nchini Cuba.
Hata hivyo safari yake iliishia Mombasa Kenya alikoanza kufanya kazi ya kuchoma mishkaki. Taarifa za Salum kuwa Mombasa zikamfikia Baba yake ambaye akafanya juhudi za kumrejesha Morogoro na hatimaye akafanikiwa. Ili kumvuta zaidi mwanawe, Baba yake alimnunulia gramaphone aliyoitumia kusikiliza nyimbo hasa za Latino. Na gramaphone hiyo alikuwa anaisikiliza pale kwenye mgahawa wa Baba yake. Pale kwenye mgahawa huo alikuwepo Mhudumu mwingine akiitwa Kibwana Seif Kata shingo ambaye naye kama Salum alikuwa na mahaba na muziki. 
 
Wawili hawa wakatafuta wenzao wengine kama akina Idd Mwanamtwa, Paul Majuto na hata Gaspar Sekulu na mwaka 1947 wakaanzisha Kundi la muziki likiitwa La Paroma. Hata hivyo baadaye kundi likabadili jina na kuitwa Cuban Marimba. Nyimbo kadhaa nzuri za bendi hii zilihanikiza anga la muziki wa Tanzania. Baadaye mwaka 1963 akaongezeka mpiga gitaa hatari kutoka Tanga wakati huo, Waziri Nyange ama Simba Mzee. Huyu ndiye amepiga solo kwenye nyimbo nyingi maarufu za Salum Abdallah kama vile Shemeji shemeji, Wanawake Tanzania, Ee Mola wangu, Kaburu Ngoma iko huku na kadhalika. Mzee huyu yu hai bado na yupo pale Buguruni sasa ni Mtaalamu wa tiba asili. 
 
Nov 18 mwaka 1965, Salum Abdallah alipata ajali ya gari ambapo gari lake mwenyewe lilimkanyaga na kusababisha kibofu chake cha mkojo kupasuka. Mazingira ya ajali yenyewe ni majira ya jioni ya saa moja. Mazingira ya ajali yanahitaji post inayojitegemea. Kesho yake yaani Nov 19, majira ya saa kumi jioni, maisha ya mwanamuziki huyu alikoma rasmi katika Hospitali ya Morogoro. Alizikwa kesho yake pale Msamvu Morogoro. 
 
Baada ya kufa Salum Abdallah, jahazi la uongozi likaenda kwa Juma Kilaza ambaye wakati huo alichukuliwa kutoka Kilosa alikokuwa amekwenda kufanya kazi kwenye Kiwanda cha Singer baada ya kuachana na Morogoro Jazz.

No comments:

Post a Comment