Front page

MATANGAZO

KARIBU

Monday, November 25, 2013

Profesa Ngugi wa Thiong'o....

NAKUTUNUKU_ce5b6.jpg
WASOMI   MPO
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania mwishoni mwa wiki kilitunuku digrii ya Heshima Mwana fasihi na mwandishi wa vitabu maarufu Afrika Profesa Ngugi wa Thiong'o.

Ngugi alitunikiwa digrii ya Uzamivu wa Fasihi "Doctor of Literature" ambayo ni ya pili kutunikiwa barani Afrika baada ya aliyotunikiwa kutoka Chuo Kikuu cha Walter Sesulu cha Afrika ya Kusini.

Raia huyo wa Kenya ambaye aliwahi kukimbilia uhamishoni baada ya maandiko yake kupingana na serikali ya Kenya sio mgeni nchini Tanzania kwani baadhi ya vitabu vyake vimeorodheshwa katika mitaala ya shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu nchini humo.Akizungumzia kuhusu heshima hiyo aliyopewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ngugi amesema amefurahishwa kwa kuwa Chuo hicho kikuu kimetambua mchango wake katika fani ya fasihi na uandishi wa vitabu.
 
Akizungumzia kuhusu waandishi vijana wanaochipukia Ngugi amesema amefurahishwa kuona na baadhi ya waandishi vijana ambao wanafuata nyayo zao kwa kuandika mambo yanayogusa jamii na kuibua mambo mazito.
Kuhusu maono ya kuandika kitabu kitakachohusu matukio yaliyotokea Kenya hivi karibuni Ngugi amesema anatafakari na upo uwezekano akaandika kitabu kinachohusu hayo yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment