NA..REHEMA LUCAS MBANDO |
Mkuu wa wilaya ya moshi Dr Ibrahimu Msengi ameitaka benki ya ushirika kilimanjaro KCBL kuongeza mtaji wake ili iweze kuwa na mafanikio zaidi ya waliyonayo sasa.Wito huo ameutoa novembar 20 mwaka huu wakati akimwakilisha mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Leonidas Gama kwenye mkutano wa kumi na tisa wa mwaka wa KCBL uliofanyika mjini moshi uliowahusisha wadau mbalimbali wa vyama vya ushirika ,wanahisa wa benki hiyo.
Dr msengi amesema kuwa ili malengo ya benki hiyo ya ushirika yafanikiwe lazima wanahisa wake wanunue na kuongeza hisa zao ili kuongeza mtaji ambapo watakua na ushawishi mkuubwa kwa benki kuu BOT kuwapunguzia vikwazo vya mashariti magumu yanayoweza kufanya kushindwa kufikia malengo yao.Amepongeza wanachama sita wapya waliojiunga na benki hiyo huku akitoa angalizo kwawanachama wote kuwa makini na walanguzi wanaotumia jitihada nyingi za kuvunja ushirika wao hasa kupitia wakulima hivyo watumie ushirika wa kcbl ili wajipatie ruzuku za kilimo zilizo bora na kwa wakati kutokana na kutoa huduma ya sitakabali ya mazao ghalani.
Naye meneja mkuu wa benki hiyo bi Elizabeth Makwabe ametoa zawadi za shukrani kwa wanachama waliofanya vizuri ambazo zimetolewa kwa upande wa hisa,kutumia huduma za mikopo vizuri,na walioweka amana kubwa zaidi ya milioni 30 huku walioshika nafasi ya kwanza na pili wamepata zawadi ya kikombe na mshindi wa tatu akipewa cheti. Aidha bi Makwabe amesema changamoto kubwa wanayo kabili ni baadhi ya wateja wanaoshindwa kulipa mkopo wanaweka kizuizi mahakamani cha kuzuia mali zao kuuzwa kufidia benki hiyo
No comments:
Post a Comment