Front page

MATANGAZO

KARIBU

Monday, November 25, 2013

mishahara ya wakubwa yapingwa

Wapiga kura nchini Uswisi wameshiriki katika kura ya maoni ili kuamua juu ya kuiwekea mpaka mishahara ya mameneja wa kampuni. Idadi kubwa ya wapiga kura wamepinga kuwekwa mpaka katika mishahara ya mameneja. Mpango huo ulipendekezwa na vyama vya kisoshalisti, cha kijani na jumuiya za wafanyakazi.Kwa mujibu wa pendekezo hilo, kima cha juu cha mshahara wa mameneja kingelikuwa mara 12 tu ya mshahara wa kima cha chini.Asilimia 63 ya wapiga kura wameupinga mpango huo. Waziri wa Uswisi anayeshughulikia masuala ya kiuchumi amewapongeza wapiga kura na amesema matokeo ya kura yataufanya uchumi wa Uswisi uendelee kuwa na ushindani..DW SWAHILI

No comments:

Post a Comment