Wazazi na Walezi nchini wametakiwa kuwapatia watoto wao
Elimu kwani huo ndio urithi pekee ambao
utawaangazia kama taa katika maisha yao ya baadae na kuweza kuwajengea uwezo wa
kujitegemea na kupambana na dunia ya
utandawazi. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Rift Valley School Bw, Henry Mallya kwenye mahafali ya tano ya darasa la saba
yaliyofanyika katika shule hiyo mjini Babati Mkoani Manyara.
Bw. Mallya alisema kuwa elimu ndio urithi pekee kwa watoto na kizazi kilichopo hivyo ni jukumu
la wazazi na walezi kuhakikisaha
wanawapatia watoto wao elimu iliyo bora na si bora elimu. Aidha alisema kwamba wazazi wanatakiwa kuwa wawajibikaji kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watoto
wao na walimu ikiwa ni pamoja na kutimiza wajibu wao wa kulipia ada kwa muda
muafaka bila kusumbuana ili shule hiyo
iweze kutiza malengo yake ya maendeleo ya kutoa elimu iliyo bora .
Mkurugenzi huyo aliendelea kuwashauri wazazi kuwa wandelee
kuwaandaa vizuri watoto wao ili wawe tayari kwa masomo ya sekondari au ufundi ambapo aliwaasa vijana nao
kuwa makini pindi wanapo kuwa wakisubri
kuendelea na masomo yao . “Mnapokuwa huko mnasubiri kuendelea na masomo yenu epukeni
tabia mbaya za kuiga kutoka kwenye makundi rika
na mzingatie maadili mema mliopewa
na walimu pamoja na walezi wenu” Alisema Mallya.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo
Mwl. Mtimilifu Ndekidemi Alisema kuwa
shule yao inajitahidi kuimarisha
mahusiano mazuri baina yake na jamii inayowazunguka pamoja na sekta nyinginezo ili kuweza kusaidia jamii na kuboresha
maendeleo ya o na Taifa kwa ujumla .Alisema kuwa kama jukumu la shule ni kutoa elimu iliyo bora na
kumwendeleza mwanafunzi kimwili na kiroho na kiakili hivyo basi wanahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa jamii hasa wazazi na
walezi ilin waweze kufikia malengo hayo.
Mkuu huyo aliwataka wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto kila wakati na kuhakikisha kuwa watoto
wao wanahudhuria shuleni muda wote wa masomo kwa kuwalipia ada mapema na
kuepuka usumbufu wa kurudishwa nyumbani mara kwa mara, wafuatilie matokeo ya mitihani yao, wakae na
watoto kwa ushauri zaidi wa mara kwa mara kuhusu matumizi mazuri ya muda pamoja
na makundi rika na na kuwaepusha na
madhara yatokanayo na utandawazi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mji wa Babati ambaye ndiye
alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo Bw. Omary Mkombole aliwapongeza
wanafunzi hao kwa kupata matokeo mazuri ambapo wameweza kufaulu wote hakuna
aliyefeli hata mmoja na aliwataka waongeze juhudi zaidi wanapoendelea na Elimu
ya sekondari. Pia Bw. Mkombole aliwaasa wahitimu hao kujiendeleza kimasomo
na wajihadhari na chips kuku pamoja na mafataki.
Nao wahitimu wa darasa la saba waliushukuru uongozi wa
shule, waalimu, wazazi na walezi kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake na kuwawezesha kushika nafasi nzuri kiwilaya,
kimkoa na kitaifa.
Pia walisema kuwa pamoja na mafanikio waliyoyapata kumekuwa
na changamoto kama vile upungufu wa vifaa vya
kujifunzia, ukosefu wa maktaba na maabara ya somo la sayansi. Hivyo wameuomba
uongozi wa shule utoe kipaumbele katika kukabiliana na na changamoto kwa
kununua vifaa vya kutosha na kujenga haraka majengo ya maktaba, maabara na
jengo la computer kwa kufundishia somo la ICT (TEHAMA).
No comments:
Post a Comment