Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, November 21, 2013

Kenya , Uingereza mh!!!!..

Mgogoro mkubwa wa kidiplomasia umeibuka kati ya Kenya na Uingereza baada ya kubainika kuwa wakuu wa London wanatekeleza njama dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake William Ruto wanaokabiliwa na kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC.

Duru zinaarifu kuwa Kenya imewasilisha pendekezo katika Kongamano la Nchi Zilizotia Saini Mkataba wa Kuanzisha ICC ikitaka 'rais wa nchi au yeyote anayekaimu nafasi hiyo asifikishwe kizimbani ICC hadi muhula wao wa kuweko madarakani umalizike.' Hata hivyo Uingereza ilijaribu kutumia ushawishi wake kuondoa pendekezo hilo la Kenya katika kikao hicho kilichoanza jana huko The Hague. Badala yake Uingereza imependekeza kuwa marais wanaoshatakiwa wapewe idhini ya kushirki katika vikao vya mahakama kwa njia ya video. Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Karanja Kibicho amesema pendekezo hilo la Kenya limerejeshwa katika ajenda ya kikao hicho baada ya malalamiko makali. 


Katika upande mwingine, Muungano wa Jubilee unaotawala Kenya umeituhumu Uingereza kuwa 'ina nia mbaya' katika hatua inazochukua kuhusu Kenya. Kiongozi wa Waliowengi katika Bunge la Kenya Aden Duale amesema baada ya kikao cha Hague bunge la Kenya litatathmini upya uhusiano wa Nairobi na London. Naye mbunge mteule wa TNA Johnson Sakaja amesema Uingereza inapaswa kufahamu kuwa zama za ukoloni zimefika ukingoni....IDHAA YA TEHRAN

No comments:

Post a Comment