Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, November 21, 2013

Je marais wasifunguliwe mashtaka ICC?

Mwendesha mkuu wa mashtaka ICC,Fatou Bensouda
Mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma utaendelea leo jijini Hague. Kwa mara ya kwanza katika historia ya kongamano hilo, mataifa ya kiafrika yatawasilisha mapendekezo yao ya kufanyia mageuzi mkataba wa Roma.  Suala kuu ni kubadili sheria za mahakama hiyo ili kuwapa kinga viongozi walioko madarakani dhidi ya kufunguliwa mashtaka katika mahakama hiyo.

Kenya ilifanya kila hali kuhakikisha kuwa pendekezo ililotoa la kuzuia marais walio mamlakani kufikishwa katika mahakama ya ICC,kuwa miongoni mwa ajenda ya mkutano huo.Hali hii imejitokeza huku utata wa kidiplomasia ukikithiri kati ya Kenya na Uingereza, Kenya ikihoji kwa nini pnedkezo la Uingereza klilikubaliwa kwenye konagamano hilo huku lile la Kenya likipuuzwa.

Uingereza ilipendekeza kuwa mahakama hiyo iruhusu baadhi ya kesi kuendeshwa kwa njia ya video.Ripoti zinasema kuwa Naibu rais wa Kenya, bwana William Ruto anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Kenya katika mkutano huo.Haya yote yanajiri huku ripoti zikisema kuwa mwendesha mkuu wa mashitika katika mahakama ya ICC Fatou Bensouda anataka Ruto azuiwe kuhudhuria vikao vya mkutano huo na kuzungumzia kesi anayokabiliwa nayo katika mahakama ya ICC.

Aidha mkutano huo umegeuzwa na kuwa kongamano ambalo nchi za Afrika zimetumia kuelezea kero lao kuhusu mahakama ya ICC, ambayo wameituhumu kwa ubaguzi wa rangi.Bensouda amewasilisha ombi la dharura kuwa Naibu Rais Ruto, asizungumzie kesi anayokabiliwa nayo wala kesi inayomkabili , Rais Uhuru Kenyatta kwenye mkutano huo.

Wawili hao wanatuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007 ambapo zaidi ya watu 1,100 walifariki. Hata hivyo mashirika ya kutetea haki za binadam yameshutumu vikali hatua ya serikali ya Kenya kumteua Bwana Ruto ambaye anakabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo kuongoza ujumbe wa Kenya.....BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment