Wednesday, November 20, 2013
Iran haina uadui na Marekani
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatullah Ali Khamenei, amesema leo kwamba nchi yake inataka mafungamano ya kirafiki na mataifa yote, ikiwemo Marekani. Kauli hii inakuja huku Iran ikianza duru mpya ya mazungumzo na mataifa yenye nguvu duniani juu ya mpango wake wa nyuklia unaozozaniwa. Akizungumza na wanamgambo wa kujitolea wa Basij mapema leo, Kiongozi mkuu wa Iran Ayatullah Khamenei amesema kwamba nchi yake haina uadui na taifa la Marekani, kwani ni sawa na mataifa mengine. Hata hivyo Khamenei amesema nchi yake haitarudi nyuma hata hatua moja kwenye haki zake za nyuklia. Ameilaumu Ufaransa kwa kuipigia magoti Israel na akaahidi kutoingilia kati mazungumzo hayo ya Geneva, ingawa akasema tayari ameshaweka masharti ya kufuatwa na timu ya wapatanishi. Ingawa wakati akizungumza hayo, wanamgambo hao walipiga makelele ya kuilaani Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment