Watuhumiwa
kesi ya mauaji ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk
Sengondo Mvungi wakiwa katika Viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam jana, walipofikishwa na kusomewa mashtaka. PICHA |
VENANCE NESTORY
Watu 10 wamefikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kumuua kwa kukusudia
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, Dk Sengondo Mvungi.Akiwasomea shtaka hilo jana, Wakili wa
Serikali, Aida Kisumo aliwataja washtakiwa hao, Chibago Magozi (32)
mfanyabiashara na mkazi wa Vingunguti Machinjioni, John Mayunga (56)
mfanyabiashara na mkazi wa Kiwalani na Juma Kangungu (29) mkazi wa
Vingunguti.
Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa
marehemu Dk Mvungi, Longishu Losingo (29) na Masunga Makenza (40) dereva
na mkazi wa Kitunda, ambaye anatuhumiwa kuwa ni kibaka mzoefu.Kisumo aliwataja watuhumiwa wengine,
Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa
Vingunguti, Zacharia Msese (33) mkazi wa Buguruni, Msungwa Matonya (30)
mkazi wa Vingunguti na Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala wilayani
Kinondoni.Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa
washtakiwa hao kwa pamoja Novemba 3, mwaka huu walifanya kosa hilo la
mauaji kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya
16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.Kisumo alidai kuwa siku ya tukio,
katika eneo la Msakuzi Kiswegere lililopo eneo la Wilaya ya Kinondoni,
washtakiwa hao kwa pamoja walimuua kwa kukusudia Dk Sengondo Mvungi.Baada ya washtakiwa hao kusomewa
shtaka hilo, Hakimu Sundi Fimbo aliwataka wasijibu kitu chochote kwa
sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina uwezo wa kulisikiliza
shtaka hilo hadi Mahakama Kuu ya Tanzania.Kwa kuwa shtaka hilo halina dhamana na
upelelezi bado haujakamilika, washtakiwa walipelekwa rumande hadi
Desemba 5, mwaka huu itakapotajwa.
Washtakiwa hao waliofikishwa
mahakamani hapo asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi na baada ya
kesi, waliondoka kwa kutumia gari aina ya Land Cruiser KX 06 EFD ambalo
lilikuwa likisindikizwa na gari aina ya Noah namba T 539CCB....MWANANCHI
No comments:
Post a Comment