Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, October 19, 2013

Meli ya Kimarekani na mabaharia yakamatwa India

Jeshi la Polisi huko kaskazini mwa mji wa bandari wa India, Tuticorin uliyopo katika Jimbo la Tamili Nadu, jana wamewakamata mabaharia waliokuwa katika meli yenye umiliki wa Kimarekani kwa tuhuma za kusafirisha silaha na risasi kinyume cha sheria katika bahari ya India.

Meli hiyo MV Seaman Guard, inamilikiwa na kampuni moja ya ulinzi ya AdvanFort yenye makao yake makuu mjini Virginia lakini imesajiliwa Sierra Leone na ilikamatwa Oktoba 12.  Waziri wa Mambo ya Nje wa India Sujata Singh aliwaambia waandishi wa habari kwamba mabaharia wanane na walinzi 25 walikuwemo katika meli hiyo waliwekwa kizuizini baada ya kushindwa kutoa nyaraka zinazowaruhusu kubeba silaha. 

Nahodha wa meli hiyo aliiambia timu ya wachunguzi kuwa meli hiyo inafanya shughuli ya kutoa ulinzi kwa kuzisindikiza meli za kibiashara ambazo ni wateja wa kampuni yao zinazosafiri katika Bahari ya Hindi iliokumbwa na uharamia. Mabaharia hao na walinzi 25 wanatoka India, Uingereza, Estonia na Ukraine. Lakini ubalozi wa Marekani mjini New Delhi umesema hauwezi kuzungumza lolote kuhusu tukio hilo. Rais wa kampuni inayohusika na meli hiyo AdvanFort, William H. Watson, amekanusha kwamba meli hiyo ilikuwa inasafiri katika eneo la bahari ya India.

No comments:

Post a Comment