Front page

MATANGAZO

KARIBU

Wednesday, October 16, 2013

EID NJEMA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu muda mfupi baada ya kushiriki Swala ya EID iliyofanyika katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi (picha na Freddy Maro).



Sala ya Idul Adh-ha yasaliwa katika Iran ya Kiislamu

Sala ya Idul Adh-ha yasaliwa katika Iran ya KiislamuSala ya Idul-Adh-ha imesaliwa leo kwa kuhudhuriwa na wananchi waumini katika maeneo yote ya Iran ya Kiislamu. Hapa mjini Tehran sala hiyo imesaliwa katika wa Cho Kikuu cha mji huu ikiongozwa na kusalishwa na Ayatullah Muhammad Ali Muvahidi Kermani, Imamu wa muda wa Sala ya Ijumaa wa hapa Tehran. 
 
 Sikukuu hii adhimu inakumbusha tukio la kujitolea na kujisabilia Nabii Ibrahim na mwanaye Ismail (as) kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu SW na kujisalimisha kwake. Waislamu huiadhimisha tarehe 10 Dhil-Hijja ya kila mwaka kwa kusherehekea na pia kwa kuchinja. 

Kuchinja ni moja ya amali za wajibu za Hijja lakini Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia ambao hawajapata taufiki ya kutekeleza amali hiyo, katika siku ya leo ya Idi huchinja mbuzi, kondoo, ng'ombe au ngamia na kugawa nyama kwa watu wasio na uwezo na wahitaji. 

No comments:

Post a Comment