Hakuna maafikiano kuihusu Syria huku Papa akitangaza siku ya maombi kote duniani Mkutano wa viongozi wa nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani, G20 umekamilika jana (06.09.2013) huku viongozi hao wakiwa wametofautiana kuhusu mzozo wa Syria na baba mtakatifu Francis akitoa wito wa maombi ya amani
Mkutano wa viongozi wa nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani, G20
umekamilika jana(06.09.2013) huku viongozi hao wakiwa wametofautiana
kuhusu mzozo wa Syria. Rais wa Urusi Vladimir Putin alidhihirisha wazi msimamo wake wa kupinga
kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya Syria kwa kusema kufanya hivyo
kutayumbisha kanda hiyo.
Rais wa Marekani Barack Obama kwa upande wake amesema ni muhimu hatua
hiyo ya kijeshi kuchukuliwa kuiadhibu Syria kwa matumizi ya silaha za
kemikali.
Obama ameelezea wasiwasi wake kutokana na kutokuwa kwa umoja kuhusu
jinsi ya kulishughulikia suala hilo kutoka jamii ya kimataifa.Putin
anawashutumu waasi nchini Syria kwa matumizi hayo ya sumu akidai
waliitumia wakitumai hilo litachochea nchi ambazo zinawaunga mkono
kuchukua hatua dhidi ya Assad.
No comments:
Post a Comment