Polisi nchini India imemkamata mmoja wa waanzilishi wa kundi la wanamgambo la Indian Mujahideen.Kundi hilo linaaminika kuhusika katika misururu ya mashambulio ya mabomu nchini India tangu mwaka 2005 ambapo mamia ya watu wameuawa.Waziri wa mambo ya ndani wa India amesema Yasin Bhatkal alikamatwa Jumatano usiku katika jimbo la mashariki la Bihar karibu na mpaka kati ya India na Nepal.
Maafisa wa India wanasema Bhatkal ambaye ni mmoja wa watoro waliokuwa wakisakwa sana ni mmoja wa viongozi wa kundi la Indian Mujahideen lenye mafungamano na kundi la waasi lenye makao yake Pakistan la Lashkar e Taiba.
Mapema mwezi huu maafisa wa usalama wa India walimkamata mwanamgambo mwingine wa kundi hilo Abdul Karim Tunda anayeaminika kuwa mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi hilo.Tunda anashutumiwa kuhusika katika kupnga mashambulio ya mabomu mjini Mumbai mwaka 1993 ambapo watu 259 waliuawa.
source.....dw swahili
No comments:
Post a Comment