Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, August 24, 2013

Nelson Mandela anapata nafuu

Ofisi ya rais wa Afrika Kusini imesema rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela wakati mwingine hali yake ya afya ni ya kutiliwa shaka lakini ameonyesha uvumilivu mkubwa wakati akisalia katika hali mbaya hospitalini.

Taarifa kutoka ofisi ya Rais Jacob Zuma imesema kuwa kiongozi huyo anapata nafuu kutokana na juhudi za madaktari wake.Mandela amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni mjini Pretoria akiwa na maradhi ya mapafu.

Zuma amewaomba raia wa nchi hiyo kuendelea kumuombea Mandela.Binti yake kitinda mimba Zindzi Mandela siku mbili zilizopita alisema baba yake anaweza kuketi bila kusaidiwa na yuko makini. Msemaji wa rais Mac Maharaj hata hivyo hakufafanua zaidi kuhusu hali ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 95.

No comments:

Post a Comment