Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, August 3, 2013

Mugabe aongoza uchaguzi Zimbabwe


Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe aonekana kuelekea kupata ushindi wa kipindi cha saba cha utawala baada ya ushindi katika uchaguzi wa bunge, ambao umepuuziwa na upinzani kuwa umesheheni udanganyifu.
Matokeo kamili yalitarajiwa kupatikana jioni ya leo Jumamosi(03.08.2013) lakini chama cha rais Mugabe cha ZANU-PF kinasema kuwa tayari kimeshinda viti 140 katika bunge, ambavyo vinatosha kuweza kuendelea na mabadiliko yenye utata katika katiba."Tumekwisha pata zaidi ya theluthi mbili ya viti. Ni wingi wa kutosha," afisa wa ngazi ya juu wa chama hicho ameliambia shirika la habari la AFP kwa masharti ya kutotajwa jina.Wakati majimbo 186 kati ya majimbo ya uchaguzi 210 tayari yamemaliza rasmi zoezi la kuhesabu kura baada ya uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatano, Chama cha Mugabe tayari kina wingi wa kutosha, kikishinda viti 137 katika bunge.
 

Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo ameliambia shirika la habari la AFP: "Wapinzani wetu hawafahamu kile kilichowasibu", na kuongeza kuwa Mugabe anaweza kushinda asilimia 70 hadi 75 ya kura ya urais.Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai ameueleza uchaguzi huo kuwa ni wa bandia na udanganyifu mkubwa na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) kimeapa kutokubali matokeo, hali inayozusha hofu ya kurejewa kwa ghasia zilizomwaga damu ambazo zilitokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.



No comments:

Post a Comment