Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, July 5, 2013

Mgawanyiko waja MBEYA!.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abas Kandoro akifungua mkutano wa majadiliano ulioleta muafaka wa jina SONGWE.

Songwe ndilo jina lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.   Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.

Kupatikana kwa jina hilo na mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro. Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.

Hata hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Rais

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa mapendekezo hayo ya RCC.

No comments:

Post a Comment