Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, July 6, 2013

KIBOKO YA MALARIA YAJA, CUBA YAJITOA KUIKOMBOA AFRIKA....

RAUL CASTRO,  KIONGOZI WA CUBA
SERIKALI imetoa dola za Marekani milioni 22.3 ili kujenga kiwanda cha kuzalisha viuadudu kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini. Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na mkuu wa kitengo cha uendelezaji wa maeneo ya viwanda wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Ernest Mnzava.

Alisema tayari eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho limepatikana huko Kibaha mkoani Pwani na kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. “Tunatarajia kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu, kwa sasa tunakamilisha kufunga mitambo, tayari kwa kazi na lengo letu ni kutokomeza malaria nchini, hivyo kupunguza vifo vya kinamama na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano,” alisema.

Alieleza kwamba kiwanda hicho kitakachozalisha lita milioni 6 za viuadudu kwa mwaka, kitakuwa cha kwanza Afrika Mashariki na Kati na kwamba Serikali ya Cuba ndiyo ilitoa utaalamu huo.

Alisema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo watanyunyizia viuadudu hivyo katika maji yaliyotuama kwa lengo la kuua mbu na mazalia yao kama njia ya kutomomeza ugonjwa huo

No comments:

Post a Comment