Kampuni ya nguo za michezo ya kijerumani Adidas imesimamisha udhamini wake kwa mwanariadha Tyson Gay kutoka Marekani, baada ya ugunduzi kuwa mwanariadha huyo alitumia madawa yasiyoruhusiwa.
Adidas ilisema ilishtushwa na taarifa hizo, lakini ikasema itatimiza makubaliano ya udhamini huo.
Wakati huo huo, maafisa wa kimataifa wa riadha wamesema kuwa ingawa kugunduliwa kuwa wanariadha mahiri kama Tyson Gay, Asafa Powell na Sharon Simpson walitumia madawa ni za kusikitisha, kunathibitisha kuwa vipimo vinafanya kazi vizuri.
No comments:
Post a Comment