Thursday, June 20, 2013
UTALII TANZANIA: Viboko wa ajabu wasiojulikana kwa watalii
Viboko wakijidai majini
Na Christopher Lilai, Mwananchi
Licha ya Bwawa la Mto Nyange kuwa na vivutio vya asili hakuna mkakati wowote wa kutangaza eneo hilo la utalii na kuiingizia Serikali mapato.
Ni kilometa 123 kutoka Kilwa Masoko yalipo makao makuu ya Wilaya ya Kilwa. Katika wilaya hiyo kuna Kijiji cha Makangaga na kuna kivutio kizuri cha utalii kwa mfano viboko wa ajabu ambao wanatii amri mbalimbali.
Wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 1525 wanaotokana na makabila ya Wamwera, Wangindo, Wamakonde, na Wamachinga ambao wanalitumia eneo hilo kama kivutio cha utalii ambalo linachangia pato la wakazi wa eneo hilo mpaka taifa kutokana na watalii wa ndani na nje.
Katika Kijiji cha Makangaga, kilometa tisa kutoka kijijini hapo, kuna Mto Nyange uliosheheni viboko wa ajabu ambao wana tabia ya ‘kucheka’ na kutii amri zinazotolewa, hakika ukifika unajua wamefundishwa, ni fursa nzuri ya utalii kama itatumiwa vyema.
Majira ya usiku viboko hao wanapenda kutembea kando ya maeneo yao kwa ajili ya kujipatia vyakula na sehemu kubwa wanakula majani na pia wana tabia za ziada.Zaidi ya miaka 100 iliyopita mto huo uliotengeneza bwawa na haukuwa na kiboko hata mmoja, wakazi wa maeneo hayo walitumia bwawa hilo kwa shughuli za uvuvi na mahitaji ya maji kwa kazi za kawaida.
Mkazi wa eneo hilo Yahaya Selemani Engema anaeleza chanzo ni mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Kimombo ambaye alikuwa mvuvi hodari kwenye bwawa hilo.Lakini siku moja alipokwenda kuvua hakurejea na historia kuanzia hapo baada ya wananchi kuona kiboko mmoja kwenye bwawa hilo.
Kila mwaka hivi sasa inakadiriwa kuwa wanafikia zaidi ya viboko 300, na kwamba wanatii amri ya ukoo wa Kimombo. Miongoni mwa maajabu ya viboko hao ni kuwa wana uwezo wa kujitokeza pindi wanapohitajika kwa maana wakitakiwa wajitokeze wadogo wataibuka wadogo na wakitakiwa wajitokeze wazee watajitokeza wazee wote waliomo bwawani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment