Sunday, June 30, 2013
Misri yaingia tena kwenye mgogoro
Misri inaadhimisha mwaka mmoja wa Rais Mohammed Musri madarakani kwa siku nyengine ya maandamano ya umma ambapo wapinzani wamedhamiria kumuondoa madarakani na wale wanaomuunga mkono wakiapa kumlinda hadi mwisho.
Vuguvugu la Tamarod, jina la Kiarabu linalomaanisha uasi, ndilo linaloendesha kampeni ya kumng'oa Rais Mursi likidai kuwa limeshakusanya saini milioni kadhaa zinazounga mkono kampeni yao na kuitishwa uchaguzi mpya. Mabango yanayowataka watu wajiunge na maandamano dhidi ya Mursi yameenea kila kipembe cha mji mkuu, Cairo, yakiwa yamebandikwa kwenye kuta na vioo vya magari pamoja na michoro ya "Juni 30."
Kuelekea maandamano ya leo, tayari watu wanane wameshauwa ndani ya wiki moja tu, akiwemo raia mmoja wa Marekani, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kutoka pande zote mbili za waandamanaji. Mursi, kiongozi wa ngazi za juu wa kundi la Udugu wa Kiislamu, ni rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri, akiwa ameingia madarakani kupitia wimbi la mageuzi la mwaka 2011 kwenye nchi za Kiarabu, ambalo lilimaliza miongo mitatu ya utawala wa kidikteta
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment