Maombi yamefanyika leo katika makanisa mbalimbali nchini Afrika kusini kumuombea afuweni Mzee Mandela anayeendelea kupokea matibabu hospitalini mjini Pretoria. Taarifa kutoka ikulu inaeleza kwamba Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94 anapumua mwenyewe pasi usaidizi wowote.
Rais Jacob Zuma ameashiria kwamba atamtembelea Mandela punde tu madaktari watakapotoa ruhusa. Hii ni mara ya tatu kwa Mzee Mandela kulazwa hospitalini katika muda wa mizezi sita iliyopita. Msemaji wa chama tawala cha ANC,Keith Khoza amesema anamini Mzee Mandela atapona.
No comments:
Post a Comment