Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, yuko hospitalini kwa siku ya nne ambako anaendelea kupatiwa matibabu katika chumba wa wagonjwa walio kwenye hali mbaya, kutokana na maambukizi katika mapafu.
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alikimbizwa hospitalini siku ya Jumamosi, na msemaji wa rais Mac Maharanji amesema hali yake haijabadilika. Serikali imesema Mandela, ambae ndie rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, yuko katika hali mbaya lakini imara.
Jana Jumatatu, mke wake wa zamani Winnie Mandela na mtoto wao Zindzi walimtembelea. Mabinti zake wengine wawili walimtembelea siku ya Jumapili, wakati mke wake wa sasa Graca Machel amekuwa nae tangu alipolazwa.
No comments:
Post a Comment