MWANAKIJIJI wa Ihanda, John Mjwanga
(36), amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa kosa la kumuuza mtoto wake wa
kiume wa miaka 10 kwa sh milioni 1.1 ili akachunwe ngozi.
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki
na Mahakama ya Wilaya ya Kyela, mkoani Mbeya na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joseph
Luambano, aliyedai kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.
Mbele ya hakimu huyo, Mwendesha
Mashitaka, Nicholaus Tiba, alidai kwamba Novemba 17 mwaka 2010 mtuhumiwa huyo
alikwenda Kasumulu kwenye mpaka wa Wilaya ya Kyela na Mbozi kutafuta wateja wa
ngozi ya binadamu.
Ilidaiwa kwamba akiwa huko mtuhumiwa
alikutana na Israel Edgar ambaye ni mfanyabiashara wa kuuza na kununua fedha za
kigeni, hivyo walikubaliana.
Mwendesha Mashitaka, Tiba, alidai kwamba baada ya
makubaliano mfanyabiashara huyo alitoa taarafa kituo cha polisi ambapo mkuu wa
upelelezi alifika eneo hilo akijifanya mteja.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka huyo,
mtuhumiwa bila kujua alikubaliana bei na mkuu wa upelelezi kisha alikwenda
kumchukua mtoto wake na kurejea kesho yake.
No comments:
Post a Comment