Wednesday, June 19, 2013
CUF YALAANI MLIPUKO WA BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA
CUF-Chama cha Wananchi kinatoa pole kwa Wafiwa na Majeruhi wa Tukio la Bomu lililorushwa kwenye Mkutano wa Chadema,uliofanyika kwenye Viwanja vya SOWETO Mjini Arusha.
Hili si sula la Siasa wala si suala la Udini wala si ukabila, haya ni mauaji. Tena ni mauaji yenye lengo la kusambaratisha Taifa letu. Kama ambavyo tumekwisha eleza mara kadhaa kupitia Mikutano tuliofanya kipindi cha Kampeni na kusisitiza juu haja ya Arusha kuwa na utulivu wa Kisasa, tunasisitiza tena kwamba ni muhimu kwa sasa Vyama vya siasa kuacha kutupiana lawama juu ya nani au Chama gani cha Siasa kimehusika na Mlipuko huo.
CUF- Inashauri ni vyema Viongozi wa Vyama tukawa Dira kwa Wanachama wetu kwa kutoa muongozo utaojenga Taifa letu na sio kuwa wachochezi wa kuligawa Taifa letu kwa misingi ya itikadi za Vyama vyetu. Suala hilI libaki katika mikono ya Serikali ili ifanye uchunguzi na hatimae itoe majibu kwa Wananchi.
Tangu kutokee maafa haya, baadhi ya Vyama vinataka kugeuza mauaji haya kuwa Mtaji wa kupatia kura kwa Wananchi jambo ambalo linazidisha machungu kwa Wafiwa. Watu waliopoteza maisha kwa mlipuko huo, ni pamoja na wato wawili waliokuwa wakitoka Madrasa , watoto hawa kwa vyovyote vile hawana Chama, na hata wazazi wao huenda wasiwe CCM,CUF au CHADEMA , vyama ambavyo vipo kwenye Ushindani wa kwania Viti vya Udiwani unaotarajiwa kufanyika June 30 2013. CUF-Chama cha Wananchi , kinaona jambo baya na halitaweza kujenga Arusha yenye Mshikamano iwapo kuna baadhi Vyama vitatumia Mauaji haya kama njia ya kupata kura toka kwa Wananchi.
Tunavishauri Vyama vinavyotumia Mauaji haya kama mtaji wa Kisiasa viache kwa maslahi ya watu wa Arusha na Nchi yetu kwa ujumla. CUF-Chama cha Wananchi pia kinatoa wito kwa viongozi wa Dini kuacha kuingilia suala la Uchaguzi kwa kutoa maelekezo kwa waumini wao kuchagua mgombea wanaemtaka wao kwa utashi wa Imani zao.
Ni vema kwa Viongozi wa Dini wakafahamu kwamba maelekezo ya kumchagua kiongozi wa kisiasa kwa utashi wa Imani yake utatupeleka mahala pabaya sana. Wananchi hawachagui Kiongozi wa kuendesha Ibada Msikitini au Kanisani, jambo hili litatuletea matatizo hapo baadae. CUF-Chama cha Wananchi kinawaomba viongozi wa Dini, kuacha jambo hilo kwa Maslahi ya Tanzania.
Ni vyema viongozi wa Dini wakijikita zaidi kutoa mafunzo ya kiimani yatayoezesha Viongozi wataochaguliwa kutoa Haki na kuwa waadilifu kwa Wataowaongoza na si kuwaelekeza waumini kumchagua mtu kutokana na Imani yake.
Mwisho CUF-Inatoa wito kwa wapiga kura wa Arusha kuwakataa wale wote wanaotumia mauaji haya kama mtaji wa kuwapatia kura.
Imetolewa na Abdual Kambaya Naibu Mkurugenzi wa Haki za binadamu,Habari na Uenezi 0719566567
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment