Front page

MATANGAZO

KARIBU

Sunday, June 16, 2013

BOMU LA ARUSHA LAVURUGA UCHAGUZI

Mama akikimbizwa hospitali kupata matibabu


Uchaguzi wa Madiwani wa Kata nne za Jiji la Arusha uliokua ufanyike tarehe 16/06/2013 umeairishwa hadi tarehe 30/06/2013 endapo hali itakua shwari.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Sipora Liana amesema uchaguzi huo umeahirishwa kutokana na sababu za kiusalama .

Hapo jana bomu lililipuka saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.

Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.  Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.

No comments:

Post a Comment