Front page

MATANGAZO

KARIBU

Tuesday, May 28, 2013

Mfanyabiashara aporwa mil. 22/-, ajeruhiwa

Na Julius Konala, Songea 

WATU sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamemvamia mfanyabiashara wa mazao, Nicolaus Ngahelevano (38), mkazi wa kijiji cha Peramiho A, wilaya ya Songea Vijijini na kumpora zaidi ya sh milioni 22 baada ya kumjeruhi kwa risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusidedit Nsemeki, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane, wakati mfanyabiashara huyo akiwa amelala nyumbani kwake na familia yake.

Alisema majambazi hayo yalimlazimisha Ngahelevano ayape fedha na kutokana na yeye kukaidi amri hiyo, yalijaribu kupambana naye ndipo yalipomfyatulia risasi sehemu mbalimbali mwilini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusidedit Nsemeki akiwaonesha wanahabari nyaya zilizokamatwa katika moja ya matukio ya uhalifu mkoani humo.

Alisema mfanyabiashara huyo baada ya kujeruhiwa alipelekwa katika hospitali ya misheni ya Peramiho ambako alitibiwa na kuruhusiwa. Alisema katika eneo la tukio kulikutwa maganda matatu na risasi moja vilivyookotwa ambavyo vimeonyesha kuwa bunduki waliyokuwa majambazi ni ya kivita.

Kamanda Nsimeki alisema polisi wanaendelea kuwasaka majambazi hao ambao walikimbia baada ya tukio hilo. Hadi sasa watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo. 
Alisema mfanyabiashara huyo baada ya kujeruhiwa alipelekwa katika hospitali ya misheni ya Peramiho ambako alitibiwa na kuruhusiwa.

Alisema katika eneo la tukio kulikutwa maganda matatu na risasi moja vilivyookotwa ambavyo vimeonyesha kuwa bunduki waliyokuwa majambazi ni ya kivita. Kamanda Nsimeki alisema polisi wanaendelea kuwasaka majambazi hao ambao walikimbia baada ya tukio hilo. Hadi sasa watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.


No comments:

Post a Comment