Barua ya kutatanisha iliyokusudiwa kutumwa katika Ikulu ya Rais nchini Marekani ikiwa na sumu aina ya Ricin imenaswa. Maafisa wa upelelezi wamesema barua hiyo ni sawa na ile iliyotumwa kwa Meya wa New York Michael Bloomberg. Ofisi moja ya barua mjini Manhattan imeinasa barua ya kwanza kabla ya haijafika katika ofisi ya meya huyo. Barua ya pili iliwasili katika ofisi ya kundi la udhibiti wa silaha mjini Washington.
Polisi imesema barua zote mbili zilihusu mdahalo unaoendelea Marekani kuhusu udhibiti wa silaha.
Kufuatia tukio la mauwaji ya mjini Newtown mwishoni mwa mwaka jana, na mengine, meya Bloomberg ameendelea kusikia katika mijadala kuhusiana na udhibiti wa silaha.
Bloomberg ametoa wito wa kuwepo uchunguzi mkali kuhusu maelezo ya mnunuzi yeyote wa silaha pamoja na kupigwa marufuku silaha kali za mashambulizi katika nchi nzima.
No comments:
Post a Comment