Uwanja wetu mpya.
Mwaka 2012 Tamasha la Jambo lilifanyika kwenye Bustani za Nyerere (Nyerere Gardens) karibu na Mzunguko wa Hoteli ya Impala, moja ya changamoto kubwa tulizopata ni nafasi ya kuegesha magari; hivyo kundi kubwa la watu hawakuweza kuhudhuria Maonesho ya Sanaa yaliyokuwa yakifanyika pale. Kutokana na hilo mwaka 2013 tutahamia eneo rasmi na kubwa zaidi ambalo litatupa sio tu nafasi kubwa ya kufanya shughuli zote za tamasha lakini pia nafasi na ulinzi madhubuti kwa maegesho ya magari na usalama wa watu. Taarifa rasmi ya eneo hili (pichani) hapa Jijini Arusha itawajia punde. Kaa nasi. |
Thursday, May 9, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment