Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, April 20, 2013

Wanaotumia laini za simu zisizosajiliwa kutozwa Sh500,000 au kufungwa


Share bookmark Print Email Rating
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA ), Profesa  John Nkoma, akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na viongozi wa Kampuni za Simu kuhusu usajili wa laini za simu Dar es Salaam jana. Picha na Rafael Lubava. 
 
Dar es Salaam

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano   mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari. Katika maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12.

No comments:

Post a Comment