Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, April 20, 2013

Vyura 4,430 wa Kihansi warejeshwa

SERIKALI imetangaza kuwa imefanikiwa kuwarudisha vyura 4,430 wa bonde la Mto Kihansi ambao walipelekwa nchini Marekani kwa ajili ya kutunzwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/14.

Alisema kurejesha vyura hao kumetokana na kumalizika kwa mradi wa kuhifadhi mazingira ya bonde la Kihansi kupitia Benki ya Dunia, Juni mwaka 2011. Waziri Hassan aliongeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, vyura hao walikuwa wamerejeshwa katika makazi yao ya asili katika bonde la Kihansi.

Waziri Hassan aliliomba Bunge lipitishe kiasi cha sh bilioni 55.6 kwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Rais na kwa fungu hilo kiasi hicho kinajumuisha sh bilioni 42.7 fedha za matumizi ya kawaida na sh bilioni 12.9 fedha za matumizi ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment