Willium Hague |
Wakati Bosco Ntaganda akitarajiwa kusomewa mashtaka yake katika mahakama
ya ICC, waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza, amesema hiyo ni
hatua moja muhimu iliyopigwa kueleka mustakabali wa usalama mashariki
mwa DRC
William Hague ambaye anafanya ziara kwenye eneo la maziwa makuu akiwa pamoja na mjumbe maalum wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Angelina Jolie, amesema hatua ya Bosco Ntaganda kupelekwa ICC na mwisho kufikishwa kizimbani ni moja ya mafanikio makubwa ambayo nchi za kikanda zimeweza kuyapata kwa kipindi kigumu cha usalama mdogo kwenye kanda ya maziwa makuu.
Hague amesema Rwanda imekuwa na mchango mkubwa kwenye mchakato huo ambao pengine unaweza kuiletea tija baadaye. "Hii ni moja ya mafanikio yaliyofikiwa na eneo zima, mathalan kukamatwa na kupelekwa Hague kwa Jenerali Bosco Ntaganda tunakaribisha maendeleo haya yote yaliyopatikana kwa kipindi kigumu. Lakini nisema tu kwamba Rwanda imekuwa na mchango mkubwa kwenye michakato hii yote." Alisema William Hague.
SOURCE DW
No comments:
Post a Comment